Wednesday, January 6, 2016

BEI YA PETROL, DISELI ZASHUKA

Mwandishi Wetu, Mwananchi

Bei ya mafuta ya taa, petroli na dizeli zimeshuka kuanzia leo. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza jana kuwa bei za rejareja zimepungua kwa Sh79 kwa lita ya petroli sawa na asilimia 4.01, dizeli Sh76 kwa lita sawa na asilimia 4.20 na mafuta ya taa Sh66 kwa lita sawa na asilimia 3.73.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Felix Ngamlagosi alisema bei ya petroli inayopaswa kuuzwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Sh1,898, dizeli Sh1,747 na mafuta ya taa Sh1,699, wakati bei ya juu itakuwa mkoani Kigoma, Uvinza ambako lita ya petroli ni Sh2,141, dizeli Sh1,990 na mafuta ya taa Sh1,942 kutokana na gharama za usafiri.

Kwa mujibu wa bei elekezi iliyopita ya Desemba 2 mwaka jana, bei za jumla kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa nazo zimepungua.

“Kupungua huku kwa bei za mafuta, kwa kiasi kikubwa kumetokana na kushuka kwa bei za mafuta katika Soko la Dunia na pia, kushuka kwa gharama za usafirishaji,” alisema.

Alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za petroli kwa bei ya ushindani, ilimradi bei hizo ziwe chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu