Monday, January 11, 2016

CHUO CHA KODI CHAIMARIKA KWA UMAHIRI WA MAFUNZO YA FORODHA NA KODI KIMATAIFA

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, Prof. Isaya Jairo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo picha) jijini Dar es Salaam juu ya Mahafali ya nane yatakayofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere tarehe 16 Januari mwaka huu, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Usimamizi wa Forodha na Kodi, Dkt. Lewis Ishemoi na  Bw. Charles Sabuni, Naibu mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala).
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna.
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.

CHUO cha Kodi kimeweza kupata hadhi kuwa kituo cha Umahiri wa Mafunzo ya Forodha na Kodi kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Issaya Jairo amesema wakati wakielekea katika mahafali ya nane chuo kimeweza kufikia hadhi hiyo.

Amesema kuwa kwenda katika mahafali ya nane chuo kimeanzisha ya shahada ya pili katika masuala ya kodi kufanya kutambulika kimataifa.

Wahitimu watakaotunukiwa vyeti, shahada na stashahada siku ya Jumamosi wamegawanyika katika kozi zifuatazo:-

1) Cheti cha Uwakala wa Forodha Cha Afrika Mashariki yaani East African Customs Clearing and Freight Forwarding Practicing Certificate (CFFPC); wahitimu 125

2) Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Basic Technician Certificate in Customs and Tax Management (CCTM); wahitimu 190

3) Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Ordinary Diploma in Customs and Tax Management (DCTM; wahitimu 131.

4) Shahada ya kwanza ya usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Bachelor of Customs and Tax Management (BCTM); wahitimu 68.

5) Stashahada ya Uzamili katika Kodi yaani Postgraduate Diploma in Taxation; wahitimu 23.

Kati ya wahitimu 564, wahitimu 199 ni wanawake na wanaume ni 338. Wahitimu wa Mahafali haya watafanya idadi ya wahitimu wa Chuo cha Kodi tangu kiliposajiliwa mwaka 2007 kufikia ya 3541.

Pamoja na kutunuku vyeti, shahada na stashahada kwa wahitimu, Mgeni Rasmi pia atatoa tuzo kwa wahadhiri wa Chuo cha Kodi waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha mwaka wa masomo wa 2014/2015. Tafiti hizi zimechapishwa katika majarida mbali mbali ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na Journal of the Institute of Tax Administration (JITA) linalochapishwa na Chuo cha Kodi (ITA).

Wahitimu waliofanya vizuri zaidi pamoja na wanafunzi wanaoendelea na masomo waliofanya vizuri zaidi nao pia watapata tuzo kutoka kwa wadau mbali mbali ili kuleta hamasa ya kujifunza kwa bidii zaidi miongoni mwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.

Kwa sasa chuo kipo katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango – Mkakati wake wa tatu wa miaka mitano (SP3) kuanzia Julai 2013 hadi Juni 2018 ambapo kinaendelea kubuni kozi mbalimbali na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza ili kukidhi mahitaji na matarajio ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na wadau wengine.

Katika mahafali haya chuo kinatoa wahitimu wa awamu ya tatu wa shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (Bachelor of Customs and Tax Management-BCTM), ambayo ni ya kipekee hapa nchini na katika ukanda huu wa Afrika.

Mgeni rasmi anayetarajiwa katika mahafali ya nne ya chuo cha kodi yatakayofanyika Januri 16 ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu