Monday, January 4, 2016

KARIMJEE JIVANJEE YAWATUNUKU WANASAYANSI CHIPUKIZI

Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Mahmood Karimjee, akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe, John Method ikiwa ni ufadhili wa masomo ya chuo kikuu baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano ya wanasayansi chipukizi Tanzania katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee, kulia akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe, John Method ikiwa ni ufadhili wa masomo ya chuo kikuu baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano ya wanasayansi chipukizi Tanzania katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Mahmood Karimjee, akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Edmund Luguku ikiwa ni ufadhili wa masomo ya chuo kikuu baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano ya wanasayansi chipukizi Tanzania katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee.
Mweyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee, wa pili (kushoto) na Mwakilishiwa Ubalozi wa Ireland, Carol Hannon (kulia) wakiwakabidhi zawadi ya vyeti vya ufadhili wa masomo ya chuo kikuu John Method (kushoto) na Edmund Luguku baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano ya wanasayansi chipukizi Tanzania katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
---
Taasisi ya Karimjee Jivanjee imewatunuku nafasi za masomo Edmund Luguku na John Method wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe kwa kuwa washindi wa jumla wa Tuzo za Wanasayansi Chipukizi za Young Scientists Tanzania kwa mwaka 2015.

Akiongea kwenye hafla ya kuaga washindi hao kuelekea Dublin Ireland, Meneja wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Devotha Rubama alisema washindi hao wawili watapata fursa ya kupelekwa masomoni na taasisi hiyo mara baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita. 

Wanafunzi hao watasafiri wiki ijayo kuelekea Dublin ambapo watahudhuria maonyesho ya kimataifa ya sayansi na teknolojia ambapo kila mwaka hufanyika mashindano yanayolenga kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupenda sayansi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyekiti wa Heshima wa kundi la makampuni ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee alisema “Tumepewa heshima kubwa sana kuweza kuwa sehemu ya tuzo za Young Scientist Tanzania kwani tunaamini kwamba elimu ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania na pia kwa sababu elimu ya sayansi inaweza kuleta fursa nzuri kitaaluma”.

Karimjee alisema japo mtazamo mkubwa wa taasisi hiyo hivi sasa ni kusaidia taasisi za elimu kwa kuboresha uwezo wake, familia ya Karimjee ilianzisha taasisi mbalimbali za misaada kwenye miaka ya 1950 kabla ya uhuru.

“Tumejenga shule nyingi, hospitali, zahanati na vituo vya huduma za jamii ambapo mojawapo ya misaada wetu mkubwa ni ukumbi wa Karimjee ambao tuliujenga na kuutoa msaada kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es salaam mwaka 1957 ukiwa ukumbi wa mji na badae likatumika kwa ajili ya vikao vya bunge na vilevile Uhuru wa Tanzania mwaka 1961 ulitangazwa kwenye jingo la Karimjee.

Karimjee ambaye ni kati ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa nchini alisema misaada mingine iliyotolewa na familia ya Karimjee ni ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Usagara (zamani iliitwa Karimjee Secondary School), Kliniki ya Karimjee iliyopo Mnazi Moja, na Hospitali ya Karimjee iliyopo Zanzibar.

Taasisi ya Karimjee Jivanjee hupata misaada ya fedha za kusaidia miradi mbalimbali ya jamii kutoka kampuni ya Toyota Tanzania ambayo ni kati ya walipa kodi wakubwa nchini hivi sasa ikiwa inasherekea miaka 50 ya kuwa msamabazaji pekee wa Toyota nchini Tanzania tangu mwaka 1965.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu