Tuesday, January 19, 2016

LOWASSA AWAPONGEZA WALIOSHINDA UMEYA MANISPAA ZA ILALA NA KINONDONI LEO

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mwenge jijini Dar es salaam leo, wakati wa alipowapongeza Wastahiki Meya wa Manispaa za Ilala na Kinondoni. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Kinondini, Boniface Jacob na Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko (kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa Mkutano uliofanyika Ofisini kwa aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, walipokwenda kuzungumza nae mara baada ya kushinda nafasi hizo. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Kinondini, Boniface Jacob.
Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wastahiki Meya wa Manispaa za Ilala na Kinondoni pamoja na Manaibu wao, mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu