Tuesday, January 12, 2016

MAALIM SEIF: HATUKO KURUDIWA UCHAGUZI WA ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa hali ya kisisa Visiwani Zanzibar, uliofanyika leo Januari 11, 2016 kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. Katika Mkutano huo, Maalim Seif amesema kuwa hana taarifa yeyote juu ya swala linalosikika kutoka kwa baadhi ya viongozi kuhusiana na kurudiwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar. PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na aliyekuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamadi amesema kuwa hana taarifa zozote juu ya swala la  kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake ametaka kura zilizobaki zihesabiwe na mshindi aweze kutangazwa.

Maalim Seif ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mstaafu Jecha Salum Jecha alikuwa hana mamlaka ya kufuta uchaguzi kutokana na hatua zote za uchaguzi.

Amesema kuwa Mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi bila kuwa na wajumbe walio wengi wanaounga mkono kile wanachotaka kuamua, hali ambayo haikufanyika wakati wa kufuta uchaguzi huo.

Maalim amesema Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha alikwenda kufuta uchaguzi bila kuwataarifu makamishna wa tume hiyo wakati siku mbili hakuweza kufika katika kutangaza matokeo ya urais, hivyo alichokifanya ni ukiukwaji wa maadili na Sheria na wanashangaa kwa Rais kushindwa kumchukulia hatua.

Maalim amesenukuu kifungu kinachomuongoza Mwenyekiti wa ZEC kinachoeleza kuwa “Kiwango cha mikutano ya ZEC ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne na kila uamuzi wa tume ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi”

Aidha Maalim Seifu amesema katika mazungumzo wanayoyafanya huko Zanzibar chini ya Mwenyekiti, Dk. Ali Mohamed Shein hana imani nayo kutokana na kile kinachojadiliwa kuwa wanakitoa wakati sio makubaliano katika kamati hiyo.

Maalim Seif amemtaka Rais Dk. John Pombe Magufuli kuingilia kati suala hili katika kuweza kupata suluhu ya mwafaka kwa amani kutokana na Dk. Ali Mohamed Shein kushindwa kuhimili mazungumzo hayo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu