Thursday, January 21, 2016

MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA MAGUFULI ARUSHA

 Ngoma za asili zikiwa zinatumbuiza katika uwanja wa KIA mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutua na ndege uwanjani hapo
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki  Magufuli
Na Woinde Shizza,Arusha
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa nchi ya Tanzania  ni tajiri na inarasilimali nyingi ,ila baadhi ya matajiri ambao ni mafisadi ndio wanasababisha nchi yetu kuonekana maskini  hivyo amehaidi kula nao sahani moja.
Aliyasema hayo  leo  wakati akiongea na wananchi wa  mkoa wa Arusha waliojitokeza  barabarani kumpokea  huku wakimuomba aendelee kutumbua majipu.
Alisema kuwa nchi ya Tanzania inarasilimali nyingi  ila kunabaadhi ya matajiri ambao wanapenda kujilimbikizia fedha wamekuwa wakifanya ufisadi na kusababisha baadhi ya wananchi kuendelea kuwa maskini  pamoja na nchi yetu kuonekana maskini.
“nasema hivi kuanzia sasa nipo tayari kulala mbele na mafisadi wote na pia nawapa onyo kali wale walimu ambao bado wanatoza ada mashuleni iwapo nitagundua mwalimu yeyote  anaetoza ela nahaidi ivi nitalala nae mbale ,na katika hili  sitalifanyia masiara ata kidogo”alisema Magufuli
Aidha aliwaambia wananchi kuwa kuanzia sasa elimu ni bure kuanzia shule ya msingi adi sekondari na serekali imeshaweka mipango hiyo tayari na imeanza kutumika.
Magufuli aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuendelea kufanya kazi na kusema kuwa wakati wa kampeni umeisha , mambo ya siasa yameisha sasa ivi ni wakati wa kufanya kazi tu na sio kitu kingine.
“nasema ivi sasa ivii ni wakati wa kufanya kazi kama nitaendelea kutumbua majipu kila mahali na sitawaonea huruma mtu yeyote mimi kazi yangu kubwa ni kufanya kazi tu na wananchi napenda kuwambia fanyeni kazi kwani hapa ni kazi tu”alisema Magufuli.
Alisema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhilifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao na kanda zao na kuwataka watanzania wote  kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.
Rais magufuli alipokelewa na mamia  ya wananchi  mbalimbali ambao walijitokeza barabarani ambapo pindi tu alipotoka katika kiwanja cha kia wananchi walikuwa wemejitokeza wengi mpaka ikamlazimu kufika katika baadhi ya maeneo na msafara wake kusimama ili wananchi waongee nae,sehemu ambazo aliweza kusimama ni pamoja na kikatiti ,usa river  pamoja na Tengeru .

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu