Friday, January 8, 2016

MBWANA SAMATTA ANYAKUA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA MWAKA 2015, AWEKA HISTORIA AFRIKA MASHARIKI

 Mwanakandanda anayesukuma gozi la kulipwa katika klabuya TP Mazembe ya mjini Lubumbashi nchini CONGO-DRC, Mtanzania Mbwana Ally Samatta, amenyakua tuzo ya mwnasoka bora wa Afriaka anayecheza ligi za ndani ya bara hilo kwa mwaka huu 2015.

Samatta alinyakua tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo Januari 8, 2015 katika hafla ya kukata na mundu iliyofanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa mjini Abuja nchini Nigeria.

Samatta amenyakua tuzo hiyo baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 127 mbeleya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, mlinda mlango mwenye mwembwe nyingi Robert Muteba Kidiaba ambaye alijikusanyia pointi 88.
Mwanasoka kutoka Algeria Baghdad Bounedjah alishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 63.

Samatta anakuwa mwanasoka wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kunyakua tuzo hiyo tangu historia ya mchezo wa kandanda iasisiwe.
Akiwa na Mazembe Samatta anasifiwa kwa umaridadi wake wa kupachika mabao muhimu na hivyo kuipatia heshima kubwa timu yake, hali kadhalika amekuwa mchezaji muhimu anapochezea timuyake ya taifa Taifa Stars.
Historia ya mwanasoka huyu inaanzia kule Mbagala wilayani Temeke jijiniDar es Salaam ambako alikuwa akisukuma ndinga na timu kali ya Mbagakla Market na kuiwezesha kupanda daraja hadi daraja la kwanza na ndipo Simba ilipomuona kipaji chake na kumchukua.

Hata hivyo mchezaji huyo mpole, hakudumu muda mrefu Simba kutokana na kiwango chake na alisajiliwa na klabu hiyo tajiri nchini Congo yaani TP Mazembe

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu