Tuesday, January 12, 2016

MENEJIMENTI YA NEC YAFANYA KIKAO CHA KUJADILI VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MWAKA 2016/2017

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguz Uchaguzi Tanzania, Kailima Kombwey akizungumza katika kikao maalum cha menejimenti ya Tume wakijadili vipaumbele muhimu kwaaajili ya utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wafanyakzi wa NEC wakifuatilia kwa makini.
Wafanyakzi wa NEC wakifuatilia kwa makini.
Kikao maalum cha menejimenti ya Tume wakijadili vipaumbele muhimu kwaaajili ya utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Na Mwandishi-NEC

Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kupitia vipaumbele kwa ajili ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Katika kikao chake cha Menejimenti kilichofanyika leo Januari 11, 2016, baadhi ya vipaumbele vinavyoendelea kujadiliwa ni uhuishaji wa Sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya uchaguzi, Elimu ya Mpiga Kura, na ujenzi wa ofisi ya Tume.

Vipaumbele vingine vinavyojadiliwa ni pamoja na miongozo na mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, mifumo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na mifumo ya uendeshaji wa Uchaguzi.

Tume imeanza mandalizi haya ili kujipanga vema ili mwongozo wa Bajeti utakapotoka, Menejimenti ya NEC iwe imekamilisha hatua zote za awali na kusubiri kuwasilisha katika ngazi husika.

Huu ni utaratibu mpya ulioanzishwa na Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha masuala yote muhimu yanakuwepo katika uandaaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Vikao hivi vya Menejimenti ya Tume ni vikao vya kawaida vinavyofanyika kila Jumatatu kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kila Idara na kujipanga kwa utekelezaji wa wiki inayoanza.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu