Wednesday, January 6, 2016

MHE.POSSI AMTEMBELEA MLEMAVU WA NGOZI ALIYEKATWA KIDOLE BI.ESTER MAGANGA LUSHOTO

 Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na Bi. Ester Maganga aliyekatwa kidole na watu wenye imani potofu alipomtembelea nyumbani kwake kumjulia hali na kumpa pole ya kupoteza kidole chake, katika kijiji cha Mlalo Wilayani Lushoto. Januari 5,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa pole kwa Bi. Ester Maganga baada ya kukatwa kidole chake na watu wenye imani potofu katika eneo la Mlalo Wilayani Lushoto Tanga, tarehe 5 Januari, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya ya Lushoto alipomtembelea Bi. Ester Maganga (kushoto kwake) aliyefanyiwa tukio la kikatili la kukatwa kidole na watu wenye imani potofu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipanda mche wa mparachichi nje ya makazi ya Bi. Ester Maganga (hayupo pichani) aliyefanyiwa ukatili wa kukatwa kidole ikiwa ni sehemu ya ukumbusho wa ujio wa Naibu Waziri.Tarehe 5, Januari, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu