Monday, January 18, 2016

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA) AFARIKI DUNIA, AZIKWA JIONI LEO JANUARI 18, 2016

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said Suleiman amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea katika pwani ya Dar es salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa. Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu, ambako baada ya kufikishwa ikaelezwa kuwa amekwishafariki.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu Upanga jirani na Makao makuu ya JWTZ na mazishi yanmepangwa kufanyika saa kumi jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Marehemu alipata kuwa Katibu mkuu wa klabu ya Simba ambako kulitokana na uchapakazi wake akapachikwa  jina la Yelstin.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu muda mchache kabla ya kuelekea makabulini kwa maziko.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU 

MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu