Ligi Daraja la Daraja la Kwanza (StarTimes League) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo kumi na mbili kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kituo cha StarTv kikitarajiwa kuonyesha moja kwa moja michezo miwili ya ligi hiyo.

Kundi A Ijumaa, Januari Mosi 2016 Polisi Dar watawakaribisha Mji Mkuu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku kesho Jumamosi michezo tisa ikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Jumamosi StarTv watakua uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kurusha moja kwa moja mchezo kati ya Ashanti United dhidi ya Polisi Dodoma, Polisi Morogoro watawakaribisha Kurugenzi FC ya Mafinga katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Kimondo FC wakicheza dhidi ya Burkinafaso kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Maafande wa Ruvu Shooting watacheza dhidi ya Mji Njombe katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli dhidi ya JKT Mlale katika uwanja wa Wambie mkoani Iringa, maafande wa JKT Kanembwa wakiwakaribisha Mbao FC katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Geita Gold watawakaribisha Polisi Mara kwenye uwanja wa shule ya Nyankumbu mjini Geita, JKT Oljoro watacheza dhidi ya Rhino Rangers uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, huku maafande wa Polisi Tabora wakiwakaribisha Panone FC katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

StarTv Jumapili wataonyesha moja kwa moja mchezo kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Karume, huku timu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) wakicheza dhidi ya Friends Rangers katika uwanja wa Mlandizi Mabatini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: