1. Unanunua nguo bila mpangilio.
Kuna watu wana nguo kama duka. Kuwa na nguo chache tu huwezi kushindana na fashion.

2. Unanunua Viatu bila mpango.
Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3. Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4. Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au Whatsaap Huo ni ujinga. Badilika.

5. Unakopa hela benki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi wa kuzalisha ndio ununue gari?

6. Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu wa sekondari unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7. Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa tu na marafiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.
kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8. Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM wewe unakenua tu huzinduki. Badilika.

9. Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10. Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au handbag au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji wa kufanya vitu vikubwa endelevu...

NB: MABADILIKO HUANZA NA WEWE
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: