Thursday, January 21, 2016

WAFANYAKAZI WA TBL MBEYA WAPATIWA ELIMU YA JINSIA

po1
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba akitoa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini
po2
Afande Prisca akiwazungukia washiriki wakati wa semina
po3
Baadhi wa wafanyakazi wa TBL Mbeya wakimsikiliza afande Prisca wakati huo huo wakipata chakula cha mchana.
po4
Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni.
---
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group katika kiwanda cha Mbeya leo wamepatiwa semina kuhusiana na masuala ya jinsia naMkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba.

Katika semina hiyo wafanyakazi waliweza kujua masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kijinsia ambapo pia walipata fursa ya kuuliza sheria na masuala ya jinsia kutoka kwa mkufunzi huyo kutoka Jeshi la Polisi.

Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki mafunzo hayo walisema kuwa yameweza kuwafumbua macho kujua masuala mbalimbali yatakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku wanapokuwa sehemu za kazi na katika maisha ya kawaida na familia zao wanapokuwa wameishatoka kazini.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu