Thursday, January 21, 2016

YALIYOMKUTA MDAU: KUWENI MAKINI MNAPOSAFIRI

"Jana nikiwa safarini tumepatwa na tukio lisilo la kawaida! Kumbe hizi ajali zingine ni nguvu za kichawi chawi tu. 

Ni hivi jana tumefika Tinde kwenye mizani ya tanroads kuna mzee akalalamika kuwa kaibiwa laptop, ikabidi gari igeuze tuelekee kituo cha police si mbali kutoka hapo! 

Police wakaamuru kila abiria atone na begi lake kwa upekuzi! Ila tukiwa singida kuna jamaa alipanda na hakuweka begi lake chini yaani mda wote alikuwa amelipakata na alikuwa siti ya jirani yangu tu.

Sasa kwenye upekuzi tulishuka nae ila begi akaliacha chini ya siti, upekuzi ulipoisha askari wakaingi ndani ya basi wakashuka na begi mbili, moja ilipata mwenyewe ila nyingine ikakosa mwenyewe, yaani moja ya ile begi mwenywwe alikua sister mmoja hivi na alijitetea kuwa alichemka kuitoa juu ya keria (zile za ndani) ile nyingine ikabidi ifunguliwe... lahaulaah! 

Kilichokutwa ndani ni tunguli,vibuyu, sufuria, vitambaa vyeusi na vyekundu, ugali na nyoka wakubwaa wawili.

Sadick Hamis - Kahama - Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu