Tuesday, January 5, 2016

ZIARA YA MHE.POSSI KATIKA VITUO, VYUO NA SHULE ZA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI TANGA JANUARI 4, 2016

Katibu Tawala mkoa wa Tanga Bw. Salim Chima (wa kwanza kushoto) akimpitisha Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi katika taarifa ya mkoa wa Tanga, wakati wa ziara yake ya kutembelea Shule na Vituo vya watu wenye ulemavu mkoani hapo, Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mtaalamu wa vifaa bandia na vifaa visaidizi vya watu wenye ulemavu Bw. Richard Mbawa akimwonesha Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi namna kifaa cha mguu bandia kinavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Chuo cha Watoto wenye Ulemavu wa Viungo cha YDPC Tanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Pongwe Bw. Yahya A. Matifa (wa kwanza kulia) akimonesha Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi maeneo ya shule hiyo wakati wa ziara yake katika shule za watu wenye mahitaji maalum mkoani Tanga.Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu