Katibu Mkuu wa Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (TPC), Peter Sarungi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, wakati akitoa shukrani zake kwa kampuni ya uuzaji wa mafuta nchini ya GAPCO, kwa kuwadhamini kwenye mashindano ya Mbio za KM10, za Kilimanjaro Marathoni kwa watu wenye Ulemavu, linalotarajiwa kufanyika kesho tarehe 28 Februari 2016, Mkoani Kilimanjaro.
---
Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee (TPC) kimepanga kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathoni zinazodhaminiwa na kampuni ya GAPCO Tanzania wikiendi hii.

Akiongea Dar es Salaam, Mr. Peter Sarungi, ambaye ni Katibu Mkuu wa TPC, akitoa shukrani zake kwa GAPCO, kampuni inayoongoza katika uuzaji wa mafuta Tanzania kwa kudhamini mashindano ya Mbio za Kilimanjaro Marathoni za KM10 kwa ajili kwa walemavu, zitawapa wanariadha walemavu nafasi si tu nafasi ya kushindana miongoni mwao lakini pia kutangamana na wanariadha kutoka sehemu mbalimbali duniani. “Tunaamini kwamba hii ni nafasi muhimu kwa TPC ili kutambua wanariadha walemavu ambao wanaweza kuwakilisha Tanzania kimataifa katika matukio mbalimbali ya kimichezo.

Alieleza kwamba mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu ambazo zinadhaminiwa na GAPCO ni shindano linalojumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa. Shinando litafanyika tarehe 28 Februari 2016 sambamba na mbio za Kilimanjaro Marathon Moshi, Kilimanjaro na usajili utaanza tarehe 26 Februari 2016. “Mbio hizi ni kwa ajili ya walemavu wote wa Kitanzania, ambapo 60 kati yao watakuwa wakidhaminiwa na GAPCO kushiriki kutoka Dar Es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar” aliongeza.

Tangu GAPCO ilipoanza kudhamini Marathon mwaka 2011, wameshuhudia maendeleo chanya mwaka hadi mwaka katika ubora wa mashindano. “ Tunashukurum jitihada za GAPCO, si tu katika kufanikisha shindano hili kupitia udhamini wake lakini zaidi ni kutoa msaada wa mahitaji maalumu kwa washiriki wenye ulemavu katika mfumo wa chakula na usafiri.” alisema MrSarungi. “Pia tunafuraha kuhusu kuongezeka kwa zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi ambapo ni Tsh. 1,000,000 kiasi hiki kinaweza kubadili maisha ya washindi.

MrSarungi amewasihi watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wanariadha watakaoshiriki mbio hizi. “Tunataraji kushiriki na tunachukua nafasi hii kuwakaribisha Watanzania kujitokeza na kuwapashangilia wanariadha wetu katika tukio hili”.

Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee [TPC]) ni chama cha kitaifa na kimataifa kinachotambulika na Serikali kupitia Baraza la Sanaa Tanzania na Chama cha ridhaa kwa walemavu cha Kimataifa (International Paralympics Committee [IPC]). TPC imekusudia kuwaleta pamoja wanariadha walemavu kutoka Tanzania kupitia matawi ya kimikoa na kiwilaya na makundi mengine yenye hulka zinazoshabihiana (shule za walemavu na timu za michezo).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: