Friday, February 12, 2016

KAZIMOTO KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUMPIGA MWANDISHI WA HABARI


Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto anasubiri kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia na kumpiga mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Mwanahiba Richard.

Kazimoto alifikishwa polisi jana na kutakiwa kuripoti leo mchana ambapo alichukuliwa maelezo yake na sasa upelelezi umeanza kufanyika ili apandishwe kizimbani. Mamlaka nyingine ikiwemo Shirikisho la Soka Tazania zinasubiriwa kutoa tamko ambapo kama atapatikana na hatia adhabu ya juu ni kufungiwa kucheza soka kwa muda wa mwaka mmoja.

Mwanahiba alipata huduma za kitabibu kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga na sasa anaendelea vizuri huku kampuni ya Mwananchi ikitoa tamko kulaani kitendo hicho.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu