Monday, February 22, 2016

KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA BARABARA KATIKA MAKUTANO YA BARABARA YA MOROGORO HASA MAGOMENI

Naomba nieleze kwa ufupi kuhusu matumizi ya barabara katika makutano ya barabara ya Morogoro/Kawawa eneo la Magomeni traffic lights. Nimeona nitoe ufafanuzi ili kusaidia uelewa kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa unapofika Magomeni traffic lights hauruhusiwi kupinda kulia (No right turn). Hivyo basi utaratibu upo kama ifuatavyo:

1. Kwa madereva wanaotokea Jangwani kuelekea Kinondoni, atapaswa apitilize kama anaelekea Ubungo hadi kwa Shekhe Yahaya atapinda kulia na kurudi hadi Magomeni tragfic light na ndipo atapinda kushoto kuelekea Kinondoni (Kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na msikiti mkubwa kabla ya kufika traffic lights). Ama unapofika Magomeni Mapipa ukitokea Jangwani utapinda kulia na na kwenda kutokea eneo la Moroko hotel karibu na Kanisa la RC utapinda kulia kuelekea Kinondoni (kuna alama ya mchoro Barabarani eneo hilo la Mapipa inaelekeza kwenda kulia kwa wanaelekea upande huo).

2. Ukitokea Kinondoni kuelekea Ubungo (kuna kibao cha maelekezo kupande wa kushoto karibu na kanisa la KKKT kabla ya kufika traffic lights)dereva atakapofika mataa atapaswa apinde kushoto kama anaelekea jangwani na atakapofika Bondeni hotel (kuna alama chini barabarani na kibao cha maelekezo) atapinda kulia kuingia brbr ya kawaida kurudi mataa ndipo aendelee na safari yake ya kuelekea upande wa Ubungo.

3. Ukitoka Kigogo round about kuelekea Jangwani (kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na petrol station kabla ya kufika mataa) dereva atapaswa apinde kushoto kama anaelekea ubungo hadi kwa Shekhe Yahaya atapinda kulia kurudi traffic lights na kuendelea na safari yake kuelekea Jangwani/Mjini.

4. Pia eneo la njia panda ya barabara ya Mabibo /Morogoro na junction ya Mikumi kwa Shekhe yahaya hairuhusiwi kupinda kulia kwa wale wanaotokea ubungo. Vibao vipo vinaelekeza namna ya kupita kwenda mabibo au mikumi.
NB. Mabadiliko hayo yanatokana na uwepo wa barabara za BRT. Madeva waliowengi wanaendesha kwa mazoea na siyo kufuata sheria za barabarani kwa maana alama na michoro iliyopo barabarani. Naamini kila dereva akizingatia na kuheshim utaratibu na alama zilizopo, hakutakuwa na tatizo lolote wala hakuna dereva atakayekamatwa. Baadhi wanaposimamishwa na askari ili waelimishwe matokeo yake wanakuwa wakali. Haki na wajibu lazima viende pamoja.
Naomba kuwasilisha.

WASAMBAZIE WENGINE UJUMBE HUU
RSA TANZANIA.

USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu