Wednesday, February 10, 2016

LEO NI JUMATANO YA MAJIVU!!

Ndipo tunapoanza kipindi cha Kwaresima.

Kipindi hiki cha Kwaresima hudumu kwa muda wa siku Arobaini (40). Ni kipindi cha kufanya Toba inayoendana na Kufunga, Kusali zaidi, Kusoma na Kutafakari neno la Mungu. Kufanya matendo mema yaani kuwasaidia Maskini, Wajane, Yatima n.k.

Kanisa limeweka kipindi cha Kwaresima kusudi tuweze kutafakari kwa kina Mateso na Kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo!

Waamini wote Wakristo na hasa Wakatoliki wanapaswa kutafakari maisha yao ili waweze kumrudia Mwenyezi Mungu.

Majivu ni Ishara ya Toba. Jumatano ya majivu tunapakwa hayo majivu kwenye paji la USO ili kutukumbusha kuwa sisi sote ni mavumbi na mavumbini tutarudi, Rejea Mwanzo 3:19 na hata Nabii Yoel 2:13 anasema tugeuze mwenendo wetu kwa majivu na gunia tufunge na kulia mbele ya Bwana, kwa maana Mungu wetu ni mwingi wa rehema naye hutusamehe dhambi zetu.

Kufunga siku ya Jumatano ya majivu ni Amri; Kila aliye na nguvu anapaswa kufunga siku hii.

Nawatakia maandalizi mema ya Kwaresma.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu