Friday, February 12, 2016

MAJANGILI WALIOTUNGUA HELIKOPTA WAHUKUMIWA JELA MIAKA 70

Watuhumiwa wanne kati ya tisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kutungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye pori la akiba la Maswa wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kumuua rubani wake, wamehukumiwa kifungo kwenda jela miaka 70.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa adhabu hiyo katika mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa kesi ya tatu inayowakabili watuhumiwa saba ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyokuwa chini ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Mary Mrio.
 
Njile Gonga (28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
 Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
 Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi leo hii.
 Watuhumiwa wakiwa ndani ya gari la polisi, baada ya kufikishwa kituo cha polisi Bariadi wakitokea wilayani Meatu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo akionyeshwa watuhumiwa wa ujangili ambao walihusika kutungua Helkopta.
 Watuhumiwa wakiwa Mahakamani.
 Hii ni kama haijawahi kutokea kwa wakazi wa Mji wa Bariadi, Kwa mara ya kwanza kufurika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya hiyo kushuhudia watuhumiwa hao.
 Watuhumiwa wa tukio la kutungua ndege aina ya Helkopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza lilitokea mnamo tarehe 29/01/2016 katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, leo (jana) wamefikishwa mahakani kusomewa mastaka yanayowakabili.
Baada ya maelezo ya wakili huyo mahakamani hapo, watuhumiwa wote wanne kati ya saba walikiri kutenda makosa hayo, ambapo wote waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kile walichoeleza kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo wakili Mlekano aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wote ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Akitoa hukumu mbele ya watuhumiwa Hakimu huyo alisema kuwa katika kosa la kwanza, pili pamoja na kosa la nne kwa watuhumiwa wote wanne mahakama imewahukumu kifungo cha maika mitano (5) kila mmoja kwenda jela.

Hata hivyo Hakimu Mrio alieleza kuwa katika kosa la tatu ambalo watuhumiwa wawili kati ya hao saba walikiri kutenda, mahakama imewahukumu kifungo cha miaka mitano (5) jela kila mmoja au kulipa faini ya shilingi Milioni 10.

Kwa pamoja watuhumiwa wote wanne watatakiwa kutumikia kifungo jela miaka 70, huku baadhi yao wakitumikia kila mmoja kifungo cha miaka 20 na wengine kifungo cha miaka 15 kila mmoja.

Katika kesi hiyo Njile Gunga ambaye anadaiwa kutungua ndege hiyo atatumikia kifungo cha miaka 20, huku akiwa anakabiliwa na kesi mbili ikiwemo ya mauaji pamoja na uhujumu uhumi ambazo mahakama hiyo haina uwezo wa kuzisikiliza.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu