Monday, February 1, 2016

MAONI: WATANZANIA TUACHE ULIMBUKENI WA KUSAMBAZA PICHA ZA OVYO KWENYE MITANDAO

Leo wakati naelekea mzigoni (kazini) nikapita sehemu ambayo ilitokea ajali usiku wa Jumamosi Jannuari 30, 2016 kuamkia Jumapili na kupoteza maisha ya Kijana Calvin R.I.P ambae sikupata kumfahamu ila watu wake wa karibu walioguswa na Kifo chake wengi nafahamiana nao, kijana ameondoka bado mdogo sana, ukiangapia picha enzi ya uhai wake lazima ikuguse lakini tunmwombea kwa mola zaidi kwani yeye amempenda zaidi.

Natoa pole kwa wafiwa, ila sasa haya mambo ya mtandao yamekuwa mengi na kusababisha Uhuru kutumika vibaya, Mtu anakurupuka kama anavyosema @geraldhando na kuanza kutuma picha za mwili wa Marehemu wakati wa ajali  kwa kwa mtazamo na Upeo wangu mdogo nadhani si sawa na haikubaliki hata kidogo, sijui niiteje hii hali... sijui ni ushamba USHAMBA...? Kwa mfano angekuwa ni baba ya mzazi au mumeo ungesambaza picha zake na Video kama mlivyofanya...? Jaribuni kuwa na Ustiri kwa mtu anapofikwa na Mauti, tusiwe na Roho za Kinyama jamani, Mijitu inasambaza tu Video na Picha utafikiri inamjua. 

Mimi mdau,
Bonventure Tryphone Kilosa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu