Friday, February 26, 2016

MAZISHI YA MWANAMUZIKI MKONGWE KASSIM MAPILI KUZIKWA LEO SAA KUMI JIONI MAKABURI YA KISUTU, DAR

Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili (Pichani kulia) baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu... Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi jijini Dar es salaam na kukuta Mzee wetu amefariki.
 
Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha "Napenda Nipate Lau Nafasi" na "Rangi Ya Chungwa" na vingine nyingi...Pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania Dance Music Association ama Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA). 
Mara ya mwisho hadharani Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.

MAZISHI YA MZEE KASSIM MAPILI NI LEO IJUMAA 26/02/2016 SAA KUMI JIONI KISUTU. MSIBA UPO MTAA MAGOMENI NA.23 MAPIPA JIJINI DAR ES SALAAM. SHIME TUJITOKEZENI WAPENDWA KUMSINDIKZA MZEE WETU KWENYE SAFARI YAKE YA MWISHO. 

KAMA UNGEPENDA KUJIUNGA NASI KWA MCHANGO BASI TUMA RAMBIRAMBI KWA HASSAN MSUMARI-KATIBU MKUU CHAMUDATA. NAMBA ZAKE 0717340533 .. 

ADDO NOVEMBER - RAIS SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA... 0744150000

Imetolewa na Addo November
 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu