Friday, February 19, 2016

MJASIRIAMALI WA BUCHA LA NYAMA AKABITHIWA VIFAA VYA KISASA NA AIRTEL FURSA

Baada ya kufanya semina ya ujasiriamali na kutoa elimu ya kuboresha mtaji kwa vijana takribani vijana 300 mkoani Morogoro, Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel kupitia Mpango wa Airtel Fursa imeendeleza na dhamira yake ya kuboresha maisha ya watanzania na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao.
Kwa kuthibitisha dhamira Airtel FURSA imemkabidhi mjasiliamali wa bucha la nyama wa mji mdogo wa Ngerengere, wilayani Morogoro, Hashim Mikidadi , vifaa vya kisasa vinavyotumika katika kazi yake, jokofu, pamoja nakukarabati bucha, vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni tisa.

Hashim Mikidadi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 aliyejikita katika shughuli za ujasiliama wakati akiendelea na elimu ya Sekondari ili kukidhi mahitaji ya shule na chakula pamoja na kusaidia wazazi wake ambao ni wazee. Akiwa Katika umri wa miaka 17 alianza kuweka akiba ya Ths. 300,000 iliyopatikana kutokana na kazi ya kufyatua na kuuza matofali. Aliamua kuzitumia pesa hizo na kuwekeza katika kilimo cha Ufuta ambapo baada ya misimu miwili ya kilimo , Hashimu alifanikiwa kupata shilingi laki Tsh 800,000 ambazo alianzisha biashara ya bucha ambayo anaendelea nayo hadi sasa.

Akiongea kwa furaha mara baada ya kukabithiwa vifaa hivyo Mjasiriamali Mikidadi , aliishukuru mungu kwa kupata msaada huu kupitia Airtel Fursa na kusema “ nilianza biashara nikiwa na mtaji mdogo ambao haukidhi mahitaji ya biashara yangu. Sikuwa na vifaa vya kuniwezesha kufanya biashara yangu kwa ufanisi lakini leo Airtel kupitia Airtel FURSA imeniwezesha na sasa naamini ntawawezesha kuendesha biashara hii na kuisadia familia yangu pamoja na jamii inayonizunguka”
“Napenda kutoa shukrani pia kwa wafanyakazi wa Airtel kwa kushiriki katika ukarabati mkubwa wa bucha langu kwani uwepo wa vifaa hivi vya kisasa katika bucha yangu ni kuhamasisha wateja wangu na wale ambao si wateja wangu wavutiwe kupata huduma kutoka katika hii” alisema Mikidadi.

Akiongea wakati wa kumkabithi vifaa hivyo, Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema Airtel inaijali jamii inayowazunguka na kuzielewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana zao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji wa kuanzisha biashara zao na mpango wa Airtel Fursa ni njia moja wapo ya kubadirisha maisha yao.

Leo unayofuraha kumpatia msaada wenye thamani ya shilingi milioni 9 ikiwa vifaa, ni pamoja na gharama za ukarabati mkubwa uliofanyika kwenye bucha hiyo ambayo kwa sasa imekuwani ya viwango vya juu katika mji wa Ngeregere .

“Airtel FURSA” ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. Unaweza pia kutuma maombi yako kwa kupitia barua pepe ya airtelfursa@tz.airtel.com. Or tembelea tovuti yetu ya www.airtel.com na ujaze fomu yako ya maombi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu