Sunday, February 21, 2016

MMILIKI WA MJENGWABLOG AKABIDHI MISAADA YA WANA-IRINGA KWA WAHANGA WA MAFURIKO


Mmiliki wa Mjengwablog.com na mwongozaji wa kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora' Maggid Mjengwa (mwenye kofia) akikabidhi mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kisinga, Ndg. Shabani Mtimbwa na Mtendaji Kata ya Mlenge, Bi. Sarah Mbilinyi misaada iliyotolewa na Wana- iringa na watembeleaji wa mtandao wa Mjengwablog.com wakiwamo wafuatiliaji wa kipindi cha ' Nyumbani na Diaspora' kinachorushwa TBC1.

Misaada iliyokabidhiwa ni pamoja na mahema 9 na magodoro mapya 20. Kuna mabegi mengi ya nguo na viatu vya watoto, wanawake, wanaume. Misaada ina thamani ya shilingi milioni tatu na nusu. Shukran za pekee kwa ndugu Ahmed Salim ' Asas' kwa kufanikisha lojistiki ya kufikisha Pawaga misaada hiyo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu