Tuesday, February 16, 2016

NAPE ATUMBUA ‘MAJIPU’ MAWILI TBC

CL2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa TBC jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC Clement Mshana.
---
Timuatimua inayofanywa na mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano imehamia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya viongozi wawili waandamizi kusimamishwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utendaji mbovu.

Waziri wa Habari, Nape Nnauye alitangaza jana kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio, Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi, Edna Rajab.

Akizungumzia hatua hiyo, Nape alisema jana kuwa kumekuwa na mlolongo wa matuko mengi ndani ya shirika hilo ambayo yanakwenda kinyume na taratibu.

“Mbali na kuwasimamisha, nimeagiza kufumuliwa kwa idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha,” alisema na kuongeza: “Kwa vile suala lao linahusu bodi, nimeagiza bodi ichukue hatua zaidi kutokana na mlundikano wa mambo mengi.”

Waziri Nape alisema pia Bodi ya TBC inayoongozwa na Profesa Mwajabu Posi itateua watumishi wengine kukaimu nafasi zilizoachwa wazi na viongozi hao. “Unajua ni lazima tuelezane ukweli, kuna mlundikano wa mambo mengi yanayofanyika ndivyo sivyo TBC, yaani ni mengi, sitaweza kutaja mojamoja, kifupi niseme tu utendaji hauridhishi, hali inayodhoofisha shirika.

Kutimuliwa kwa wakurugenzi hao ni mwendelezo wa kasi ya Rais John Magufuli ambaye tangu ameingia madarakani, yeye na mawaziri wake wamekuwa wakiendeleza falsafa ya kutumbua majipu, kiasi cha kuwaweka matumbo joto watendaji wa taasisi na idara mbalimbali za Serikali.

Kutimuliwa kwa mabosi hao, kumekuja baada ya kikao cha Waziri Nape na Bodi ya TBC kilichofanyika Januari 13 kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo na jinsi ya kuzitatua.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mkuu TBC, Clement Mshana alisema watatekeleza maagizo hayo ya waziri na kuwataka watendaji wengine wa TBC kufanya kazi kwa bidii.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu