Friday, February 12, 2016

NENO LA LEO: NDOA SI KIFUNGO

Na Zourha Malisa.

(Pichani ni Mwanadada Zourha Malisa mara baada ya kufunga ndoa na Bw. Dickson mwaka jana Februari 7, 2015... Leo katuletea ujumbe mwanana ambao ni fundisho kwa vijana na wanandoa).
---
Baadhi ya wasichana wengi wanatamani siku ya kuvaa hilo vazi jeupe, mbaya zaidi wengine bila ya kufikiria maisha baada ya siku ya kuvaa hilo vazi yatakuaje, Maisha ya ndoa ni matamu sana kama tu uamuzi wako wa kuolewa ulikuwa ni uwamuzi sahihi na mtu sahihi, usikimbilie kuolewa kama fashion kwa maana maisha utayaona machungu, na kuichukia ndoa. 

Mwanamke mwenye busara ataendelea kufanya maisha ya ndoa kuwa yenye furaha kila siku kwa kuomba na kusali. 

Unatakiwa kumuamini mumewako, mmpe nafasi ya mambo yake binafsi ikiwemo kukutana na marafiki zake kwani maisha ya ndoa si utumwa. Kazi kubwa ni kuendelea kumuombea mumeo, upendo uzidi kitawala huku busara ikiwaongoza. Kwa wale ambao bado hawajaingia kwenye mahusiano ya ndoa. Muombee sana mwenza wako.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu