Thursday, February 25, 2016

STARTIMES YAZINDUA HUDUMA ZAKE KATIKA MIKOA MIPYA MINNE

Mratibu Mwandamizi wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Abdulkadir Mbeo (wapili kulia) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za matangazo ya kidijitali katika mikoa minne mipya ya Geita, Njombe, Katavi na Simiyu, iliyofanyika mkoani Geita hivi karibuni. Wengine ni wawakilishi kutoka serikalini. (Picha na mpiga picha wetu). 
---
Na Mwandishi Wetu,

Katika kufanikisha azma yake ya kusambaza huduma za matangazo ya dijitali kila pembe ya Tanzania, kampuni ya StarTimes Tanzania imezindua huduma zake kwa njia ya dishi (satelaiti) katika mikoa mipya minne ya Geita, Njombe, Katavi na Simiyu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumzia juu ya hatua hiyo kubwa waliyoipiga Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini, Bw. Lanfang Liao amebainisha kuwa kupeleka huduma zao katika mikoa hiyo mipya ni mpango wa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na huduma za matangazo bora ya dijitali kwa gharama nafuu.

“Mikakati yetu ni kuendelea kuiunga mkono serikali katika sekta ya utangazaji kijiditali na tukilenga haswa katika kuifikia mikoa mingi zaidi ili kutanua huduma za matangazo ya kidijitali kupitia dikoda za dishi na kuwawezesha watu wengi zaidi kufurahia matangazo hayo.
“Tutaendelea kwa jitihada zote kuiunga mkono serikali katika sekta hii wananchi wengi zaidi wapate fursa hii ya kupata matangazo na kuweza kuangalia chaneli mbali mbali zikiwa ubora mkubwa wa picha katika dikoda zetu,” alisema Bw. Liao.

Naye kwa upande wake, Mratibu Mwandamizi wa kampuni hiyo, Bw. Abdulkadir Mbeo alibainisha kuwa alipata nafasi ya kutembelea vikoa hiyo mine na muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa katika kupokea huduma hiyo wakifurahia matangazo hayo ya kidijitali katika nyumba zao.

“Tunajivunia kuweza kuongeza wigo wa soko letu katika mikoa hii minne lakini pia kutokana na kuungwa mkono na serikali tumelenga kuhakikisha kuwa huduma zetu za matangazo ya kidijitali zinafika katika mikoa yote nchini na hili linakwenda sambamba na dhima yetu ya kuona huduma zetu zenye gharama nafuu zinafika kila nyumba nchini,” alisema Bw. Mbeo.

Alibainisha kuwa zoezi hilo la usambazaji wa dikoda hizo za dishi katika mikoa hiyo lilikuwa la ufanisi mkubwa kwa kusambaza dikoda 500 katika kila mkoa.

“Wakazi katika mikoa hii sasa wanaweza furahia chaneli zetu zenye maudhui bora ikiwa ni pamoja na kuangalia taarifa za habari, vipindi vilivyoandaliwa nchini, vipindi vya utamaduni na michezo ambapo ligi kubwa za mpira wa miguu zinaonyeshwa laivu kama Bundesliga, Serie A na Liki Kuu ya Ufaransa. Tunahitaji watu wetu kufurahia maisha ya kidijitali,” aliongeza.

1 comment :

Anonymous said...

Wilaya ya Makete Mbona haipatikani hiyo star times.na kama inapatikana frequency IPI na tp IPI. Msaada wapendwa

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu