Saturday, February 27, 2016

TOVUTI YA PROIN PROMOTIONS YAVAMIWA, KURUDI HEWANI MARA BAADA YA TATIZO KUSHUGHULIKIWA

Tunasikitika kuutangazia umma wa watanzania na wadau wetu kwa ujumla kuwa tovuti yetu ya www.proinpromotions.co.tz imevamiwa na watu wanaojiita Classic Flame kwa kitaalamu kunaitwa Hacked.

Timu nzima ya Proin Promotions Ltd inapenda kuwataarifu kuwa wadau wetu kuwa tunalifanyia kazi na kuhakikisha tunaongeza ulinzi katika tovuti yetu na kuirudisha hewani. Tunatarajia baada ya kuirudisha hewani itakuwa imara zaidi na zaidi na tunaamini hii ni changamoto tu katika sekta ya teknolojia.

Tunawaahidi kuwa tovuti yetu itarudi hewani mara baada ya wataalamu wetu kulishughulikia hilo tatizo kwani ni tatizo ndogo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu