Sunday, February 14, 2016

UKIONA UMEJIANDAA SANA NA VALENTINE BASI UHUSIANO WAKO UNA UFA

Unasubiria Jumapili ya Tarehe 14 kwa nguvu sana ILI IWEJE??? Labda kama ni Anniversary's ya penzi lenu (mlikutana siku ya tarehe hiyo) kwamba ni muhimu kuadhimisha..

Mwaka mzima ulikuwa wapi??

Watu wenye Mapenzi STRONG siku ya Jumapili ni ya kawaida kabisa na wataenda out kama hamna kinachoendelea, ila WEWE na uhusiano wako wa Bagia na Chumvi ndo unataka Ufufukie Jumapili..

Halafu Jumapili Mzike tena mpaka mwakani.

Valentine ni kila siku... Ukikuta nguo nzuri inayomfaa mwandani wako unanunua unampelekea, hata kama ni November 19... Akiona kiatu kizuri ananunua anaku-surprise hata kama ni August 7.

Penzi lililokufa halitakuwa booster na Valentine Day kamwe... Kama hupendwi hupendwi tu, Penzi halifufuki Jumapili... Penzi lililojengwa kwenye misingi Imara huenjoy Valentine kila siku.

Ukiona umepania sana Jumapili ujue Penzi lako lina shida kwa sababu hata LEO inaweza kuwa Valentine yako ukiamua.

Penzi la kweli halina tarehe kama Kalenda.nimewaza tu

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu