Wednesday, March 9, 2016

AJALI MBAYA YATOKEA TABATA MATUMBI JIJINI DAR

Alfajiri ya leo Jumatano, daladala linalotokea Gongo la Mboto kuelekea Mawasiliano limegongana na lori lilivyokuwa limebeba Ng’ombe na lori la mizigo, ajali hiyo imetokea eneo la Darajani kabla ya kufika Tabata Matumbi.

Mmoja wa shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema kuwa daladala ilikuwa imejaza abiria na baada ya kufika eneo hilo yaligongana na kusababisha vifo vya baadhi ya abiria waliokuwa katika daladala hiyo.

Mwenye ndugu jamaa au rafiki anayeishi Gongo La Mboto na anafanya kazi Ubungo au alikuwa akielekea Ubungo alfajiri ya leo... amtafute huyo ndugu jamaa au rafiki yake kujua kama ni mzima au laaah...

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu