Wednesday, March 2, 2016

HEINEKEN TANZANIA YAIPONGEZA KAJUNASON BLOG (HABARI NA MATUKIO)

Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania, Michael Mbungu akikabidhi zawadi kwa mkurugenzi na mmiliki wa Kajunason Blog (HABARI NA MATUKIO), Cathbert Kajuna ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuweza kufanya kazi vizuri kwa kipindi cha mwaka 2013/2016. Sherehe ya kukabidhi zawadi hiyo ilifanyika hivi karibuni makao makuu ya ofisi ya Heineken Tanzania zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam. Katika hafla hiyo jumla ya vyombo vya Habari vipatavyo vitano vilizawadiwa.

Baadhi ya wafanyakazi wa Heineken Tanzania, Bethuel Kinyori (kushoto) na Fredda Magombe (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi na Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna mara baada ya sherehe kumalizika.
---
 Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania, Michael Mbungu amevipongeza vyombo vya habari nchini Tanzania kwa moyo wao wa kuwafanya nao kazi mpaka wakafanikiwa kulifikia soko la Tanzania.

Akizungumza katika sherehe iliyofanyika hivi karibuni ya kuvipongeza vyombo vya habari vilivyofanya kazi nao vizuri  kwa mwaka 2013/2016, Bw. Mbugu alisema kuwa amefurahishwa kuona vijana wanavyojitoa kuwa wazalendo kuyapokea makampuni na kuweza kuyatangaza.

"Heineken Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za pekee kwa Moyo uliotuonyesha wa Ukarimu, hatuna zaidi ya kuwapa zaidi ya kusema shukrani sana... Tuendelee kuungana Mkono msitutupe," alisema Mbungu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu