Monday, March 21, 2016

MABONDIA MADA MAUGO NA ABDALLA PAZI (DULLA MBABE) KUZIPIGA MARCH 27 JUMAPILI YA PASAKA

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA waendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Pasaka march 27 uwanja wa ndani wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumzia mpambano huo mratibu wa pambano hilo, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayari kwa kuwa wapo na afya tele na wanaendelea na mazoezi yao ya mwisho mwisho kila mmoja akijitamba kumsambaratisha mwenzake ambapo mabondia mahasimu Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ule wa mwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe.

Mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi ambao wametafutana kwa mda mrefu na sasa watamaliza ubishi siku ya jumapili hii.

Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote watapima uzito siku ya jumamosi pale katika ukumbi wa Mango Garden na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka March 27 uwanja wa ndani wa Taifa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu