Tuesday, March 8, 2016

MGOMBEA URAIS MAREKANI DONALD TRUMP ATAKA WENGER AFUKUZWE KAZI HARAKA..

BILONEA na Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amemtaka kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuondoka katika klabu hiyo kwa kuwa ameshindwa kuipa mafanikio timu hiyo.

Trump ambaye anasifika kwa kuongea sana, amesema kuwa toka klabu hiyo ilipopata mafaniko mwaka 2004 hadi sasa hawajawai kufurahia uongozi wa Arsene Wenger katika klabu hiyo.
Aidha, Trump ameitaka bodi ya klabu ya Arsenal kumfukuza kocha huyo na kuhaidi kuwa yupo tayari kuhusishwa katika malipo ya mshahara wa kocha mpya atakayeleta mafaniko katika klabu hiyo hata kwa kipindi cha miaka 50 ijayo.

Amesema kuwa anashangazwa na kocha huyo kuifanya Arsenal kama mali yake bila kujua kuwa mamilioni ya mashabiki wa klabu hiyo duniani kote akiwemo yeye anaumia na matokeo mabovu ya klabu hiyo.

“Mimi ni shabiki mkubwa namba moja wa klabu hii, kama mashabiki wengine wa Arsenal siridhishwi na jinsi huyu kocha anavyoiongoza klabu yetu, haiwezekani klabu za Manchester United na Chelsea zikawa zinapata ushindi wa nyumbani na ugenini dhidi yetu,hata hawa Swansea ni timu ndogo sana lakini iweje wapate matokeo dhidi ya timu imara kama yetu?

Trump ni shabiki wa kutupwa wa washika bunguki hao,na amekuwa mmoja ya wahanga wa matokeo mabovu yanayoikabili timu ya Arsenal kwa kipindi kirefu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu