Saturday, March 12, 2016

MKUTANO WA CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO TANZANIA (TDA) NA WAANDISHI WA HABARI NA WADAU KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO HAYO 20, MACHI 2016 MKOANI MOROGORO

  Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akifungua mkutano huo
  Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akisalimiana na Mkuu wa Huduma za Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto  Dr. Ahadiel Senkoro kabla ya kuanza kwa Maadhimisho hayo
 Wadau wakifatilia kwa makini wakati alipokuwa akiongea Rais huyo
  Mkuu wa Huduma za Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto  Dr. Ahadiel Senkoro kabla ya kuanza kwa Maadhimisho hayo akisalimia.
 Mkuu wa Idara ya Meno, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk, Rachel Mhavile akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya  Maadhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani yatakayofanyika mkoani Morogoro Machi 20,mwaka huu.kushoto ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro na  Makamu wake, Dk. Ambege Mwakatobe.
NA KHAMISI MUSSA
CHAMA cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), kinatarajia kufanya matembezi katika shule mbalimbali za watoto wenye mahitaji maalum zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro ikiwa ni katika kuadhimisha maadhimisho ya kinywa na meno.

Hayo yalisemwa na Rais wa TDA, Dk. Lorna Carneiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alibainisha kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni 'afya njema ya kinywa ni afya ya mwili mzima'.

Dk. Carneiro, alisema Machi 14 hadi 19 madaktari watatembelea shule ya mahitaji maalum ya Mtoni Maalum, Sinza Maalum, Buguruni Maalum na zingine za Mkoa wa Morogoro ambapo pia watafanya uchunguzi na matibabu.

Alisema katika siku ya kilele TDA itatoa huduma ya uchunguzi wa kinywa na meno kulingana na mahitaji katika Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege ambapo mgeni rasimi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Rais huyo alisema pia chama hicho kitatoa elimu, uchunguzi na matibabu ya kinywa na meno kwa waototo wenye ulemavu wa ngozi walioko Buhangija Shinyanga.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu