Thursday, March 24, 2016

MSHANA AWAAGA WAFANYAKAZI TBC NA KUMKARIBISHA MKURUGENZI MKUU MPYA DK. AYOUB RYOBA.

MSH1
: Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkaribisha rasmi katika ofisi za shirika hilo na kumkabidhi rasmi ofisi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba leo jijini Dar es Salaam.
MSH2
Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk.Ayoub Ryoba akitia saini kitabu cha wageni Baada ya kukaribishwa na kukabidhiwa rasmi ofisi za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
MSH3
Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba Taarifa ya Makabidhiano ya ofisi leo jijini Dar es Salaam.
MSH4
Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana akizungumza jambo wakati wa sherehe za kuwaaga wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) na kumkaribisha mkurugenzi mkuu mpya Dkt.Ayoub Ryoba (wa pili kulia) leo jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TBC Balozi Herbert E.Mrango na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Bi.Elimbora Muro (wa kwanza kushoto).
MSH5
Wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) wakimskiliza Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba (hayupo Pichani) wakati alipokuwa akiongea nao leo jijini Dar es Salaam.
MSH6
Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk.Ayoub Ryoba akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo(hawapo pichani) wakati wa kumuaga mkurugenzi mstaafu wa shirika hilo Bw.Clement mshana.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu