Thursday, March 17, 2016

MWANZA ‘MJI WA KIPEKEE WENYE MANDHARI YA TOFAUTI’

Mwanza, mji wa pili kwa ukubwa unaokua kwa kasi kimaendeleo na hasa katika sekta ya utalii Tanzania. Wakazi wake wengi ni wazawa wa kabila kubwa zaidi Tanzanzia la Wasukuma, mji huu umekuwa ukikua kwa kasi ambapo kwa sasa ni maarufu kama Rock City (Mji wa Miamba) kutokana na jiji hili kuzungukwa na miamba mikubwa iliyochomoza katika sehemu mbalimbali ikiwamo milimani na Ziwani.

Kwa uzuri na ukubwa wa miamba, Jovago Tanzania imeona hiki ni kivutio kikubwa hasa kwa watalii wengi ndani ya mji huu, ambapo kuna mwamba maarufu uliopewa jina la ‘Bismark Rock’. Ni maajabu makubwa kwa namna ambavyo mawe mawili makubwa yameweza kubebana, bila kuanguka hata nyakati za upepo na mvua kali, kwa kipindi cha miaka mingi.
Ikiwa wewe ni mpenzi wa kutalii, JovagoTanzania imegundua kuwa mji huu umekuwa ni wa kipekee wenye utulivu na madhari ya tofauti:

Uwepo wa Mbuga za wanyama; Bado utafurahia uwepo wako Mwanza, usikose kutembelea kisiwa cha Rubondo ambacho kina mbuga nzuri ya wanyama na kuweza kufurahia safari za kitalii kwa kiwango cha juu. Kinachovutia zaidi katika safari ya kwenda Rubondo, ni kuanza safari kwa kutumia boti ndogo, japo unaweza kutumia usafiri wa anga. Ukiwa Rubondo utaweza kuwaona Tembo, Kiboko, Swala, Nyani, na mamba na wengine wengi wakiwemo jamii tofauti ya ndege.
Hifadhi ya Taifa Rubondo

Ukipata muda wa kutosha, ukiwa Mwanza unaweza kupanda boti kutembelea kisiwa cha Saa Nane. Ni kisiwa kidogo ndani ya Ziwa Victoria, chenye wanyama wa kufugwa(zoo) kama Nyani, Simba na Fisi, na Watanzania wengi hutembelea kisiwa hiki siku za mapumziko ili kupunga upepo.
Ziwa Victoria linapatikana Mkoani hapo lina vivutio vingi vya utalii vikiwemo visiwa, fukwe na hoteli zenye mazingira nzuri machoni. Lakini pia, unaweza kutumia Ziwa Victoria kama usafiri wa kutembelea nchi jirani kama Uganda na Kenya.

Usisahau kufanya ziara kwenye masoko maarufu jijini Mwanza. Masoko yenye kila kitu, kama unataka vyakula, ngoma za tamaduni, vito vya kimaasai, viungo na bidhaa nying za sanaa.

Ikifika jioni, unaweza kwenda kutazama machweo ya jua ziwani, pia tembelea Bwiru sehemu yenye mazingira yanayovutia zaidi Mwanza, penye umaarufu wa jina la ‘Miamba Inayocheza’ (Dancing Rocks), Bwiru ni moja ya sehemu itakayokutengenezea kumbukumbu za pekee kuhusu Mwanza.

Ukiwa Mwanza unaweza kuchagua kuishi na kutembelea katika Hoteli na kambi za bei nafuu ambazo kwa thamani ya pesa na huduma inayopatikana, ni nafuu sana.
Malaika hoteli.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu