Tuesday, March 8, 2016

NAPE:TUTATENGENEZA SERA MADHUBUTI ILI SEKTA YA FILAMU IWE RASMI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea Tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili barani Afrika ambayo imetwaliwa na msanii Single Mtambalike a.k.a Richie (katikati, kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na wapili kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) leo jijini Dar es Salaam.Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah, Mwambene(kushoto) na kulia ni Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kiswahili barani Africa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia waliokaa ni Msanii Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kishwahili barani Africa, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Msanii Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kiswahili barani Africa akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa Filamu walioiwakilisha nchi katika mashindano ya Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) leo
jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na Msanii wa Kitanzania anayeishi Marekani Honey Moon. Hafla hiyo imeambatana na kukabidhiwa vyeti vyapongezi kutoka Serikalini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah ,Mwambene akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.Ambapo wasanii hao walikabidhiwa Vyeti vya pongezi na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wao katika kukuza tasnia hiyo hapa nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kutwaa Tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili Barani Afrika msanii Single Mtambalike a.k.a Richie leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.Tuzo hiyo imetokana na mashindano ya Tuzo za Fiolamu za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) yanayofanyika nchini Nigeria ambapo wasanii sita kutoka Tanzania walishiriki na wawili kuibuka na ushindi ambapo mshindi mwingine ni Lulu Michael.aliyeshinda Tuzo ya Filamu Bora Afrika Mashariki.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses akimkabidhi cheti cha pongezi Mwakilishi wa Kampuni ya Prion Promotion Josephat Lukaza kwa Filamu zilizotengenezwa na kampuni hiyo kutwaa Tuzo za Filamu Bora ya Kiswahili Barani Afrika iliyotwaliwa na msanii
Single Mtambalike a.k.a Richie na Filamu Bora Afrika Mashariki iliyotwaliwa na Lulu Michael leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses akimkabidhi cheti cha pongezi mama wa msanii wa Filamu Monalisa, Suzan Lewis ikiwa ni kutambua ushiriki na uwakilishi wa Monalisa katika mashindano ya Tuzo za Filamu za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) yanayofanyika nchini Nigeria.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses akimkabidhi cheti cha pongezi kwa msanii HoneyMoon Mohamed kwa kushiriki na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Tuzo za Filamu za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) yanayofanyika nchini Nigeria.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses akimkabidhi cheti cha pongezi Mwakilishi wa Kampuni ya Kijiweni Production kwa kushiriki na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Tuzo za Filamu za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) yanayofanyika nchini Nigeria.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa ana Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Filamu Tanzania mara baada ya zoezi la kutoa vyeti vya pongezi kwa wasanii walioshinda Tuzo za Filamu za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) ambapo Single Mtambalike alishinda Filamu Bora ya Kiswahili Bara Afrika na Lulu Michael Muigizajji Bora wa Kike katika Filamu za Kiswahili.Picha na Frank Shija, WHUSM.
---
---

Na Daudi Manongi.

Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amewahaidi wasanii kuwa atatumia ushawishi wake ili kuifanya sekta hii iwe rasmi kwa kutengeneza sera nzuri.

Mhe Nape ameyasema hayo wakati alipokuwa akiwapongeza washinda wa Tuzo za Filamu Bora zilizoandaliwa na African Magic viewer’s choice(AMVCA) mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Hongereni sana kwa heshima kubwa mliyoiletea nchi yenu,ushindi huu ni wa watanzania wote,mwonekano wenu ulikuwa mzuri,maneno yenu yalikuwa yenye heshima kubwa mbele za watu,nashkuru kwamba kabla ya kuondoka mlikuja kuaga na sasa mmeshinda muendelee na moyo huo huo wakuja kushukuru mnapofanikiwa.”Alisema Nape.

Aidha Waziri uyo aliwaambia wasanii hao kuwa serikali ya awamu ya tano ina nia njema ya kuwasaidia na ivyo atatumia dhamana aliyonayo kama waziri kutengeneza Sera ili ilete sheria,kanuni na taratibu na mwisho sekta hii iwe rasmi na kila mtu alipwe kwa jasho lake kwani kuna waporaji sana wa haki za watu,tumetangaza vita tutashinda hili bila woga.

Pia waziri nape amesema kuwa serikali ina mpango wa Kuandaa kikao kati ya wasanii wa Tanzania na wanaijeria ili wabadilishane mawazo na uzoefu ili tasnia hii isonge mbele Zaidi.

Naye Mshindi wa Tuzo ya filamu bora ya lugha ya Kiswahili Single Mtambalike ameipongeza wizara ya Habari,utamaduni,Sanaa na michezo na hasa Waziri Nape kwa ufuatiliaji wake wa karibu mda wote wakiwa naijeria kuhakikisha wanapata mapokezi mazuri na kumwomba waziri uyo kushughulikia kwa haraka suala la sera kwani tasnia hii ya filamu ni ajira tosha kwa watanzania akitolea mfano nchi ya Nijeria kuwa tasnia ya filamu inashika namba mbili kwa kutengeneza ajira na kuwaomba watanzania kuweka uzalendo mbele kwa kununua kazi za nyumbani kabla ya za nje uku lengo kuu likiwa kutengeneza filamu zenye ubora mkubwa ili zishindane na kuwa namba moja.

“Wenzetu wana fursa nyingi,wanapata support kubwa sana kutoka serikalini kwao na makampuni binafsi hii yote ni sababu wana sera nzuri”Aliongeza Mtambalike.

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba amesema kuwa amejiskia faraja kupata nafasi ya kukutana na waziri kwani toka apewe wizara hii amekuja na nyota isiyo ya kawaida,rekodi yake imekuwa kubwa sana,wana matumaini nae na wana imani kupitia waziri uyu wanaweza kufika mbali.

“Tumuombee waziri ili tuweze kuvuka,tumekuwa wa pili kama wazalishaji afrika,tatizo kubwa ni ubora wa filamu zetu,tunaiomba serikali itusidie katika hili ili mwakani tulete tuzo saba,tumechoka kuonewa na sasa tunataka nafasi yetu.”Alisema mwakifamba.

Pongezi hizi zimekuja baada ya wasanii kutoka Tanzania Single mtambalike na Elizabeth Michael kushinda tuzo za Africa Magic Viewer’s choice Awards kwa vipengele vya Filamu bora ya Kiswahili afrika na filamu bora afrika Mashariki.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu