Tuesday, March 8, 2016

NMB YAKABIDHI MILIONI 25 KWA TIMU YA TAIFA MPIRA WA MAGONGO

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari katika hafla ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 kukabidhiwa bendera na udhamini wa Benki ya NMB. Benki ya NMB imetoa Shilingi Milioni 25 pamoja na mabegi kwa kila mchezaji anayekwenda kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (wa pili kulia) akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) moja ya mabegi iliyotoa kwa ajili ya wachezaji wa Timu ya Taifa Mpira wa Magongo chini ya miaka 21. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akishuhudia tukio hilo. 
 Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) akiliangalia moja ya
mabegi yaliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya
Mpira wa Magongo chini ya miaka 21. Timu hiyo inayoelekea nchini Namibia
kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo chini ya
udhamini wa NMB
 Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 25 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) ikiwa ni fedha ya udhamini wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inayoelekea Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akipokea kwa niaba ya timu hiyo. NMB mbali ya udhamini huo imetoa mabegi maalumu kwa kila mchezaji wa timu hiyo kwa ajili ya safari
hiyo.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikabidhi bendera kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21, Elieza Jeremiah (wa pili kushoto). Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akishuhudia tukio hilo. Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inaondoka nchini Machi 3, 2016 kuelekea nchini Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo chini ya udhamini wa NMB.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 nchini Tanzania wakipiga picha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye pamoja na viongozi wao mara baada ya kukabidhiwa bendera ya taifa leo jijini Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu