Wednesday, March 23, 2016

POLISI NCHINI KENYA WAMTIA MBARONI MTU MMOJA NA PEMBE 39 ZA TEMBO

Polisi wa Kenya siku ya Jumanne walimtia mbaroni mtuhumiwa wa pembe za ndovu na kupata pembe 39 za tembo kutoka kwa nyumba yake.

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (CID), Ndegwa Muhoro, alisema Thomas Muhoro Ngatia mwenye umri wa miaka 35, alikamatwa baada ya polisi kuvamia nyumba yake katika mtaa wa Ruiru, mashariki mwa Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

"Nyumba inaaminiwa kuwa inamilikiwa na dada ya Ngatia ambaye anaishi Uholanzi," Muhoro alisema na kuongeza yeye anafanya ualifu pamoja na Wanigeria ambao wanawinda tembo.

Wakazi walisema mtuhumiwa kawaida yeye ufika nyumbani kwake usiku na "ufanya mambo peke ".

Muhoro alisema wataalamu kutoka Kenya Wildlife Service wata fanyia uchuguzi pembe za ndovu ili kujua chanzo cha tembo.

Kenya imetambuliwa kama njia kubwa ya kusafirisha pembe za tembo Afrika.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu