Tuesday, March 29, 2016

RAIS MAGUFULI AMWAPISHA MKUU WA MKOA MPYA WA SONGWE LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshuhudia Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiweka sahihi katika hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim  na  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016. Kulia ni mume wa mkuu huyo wa Mkoa Bw. Juma` Boma na kushoto ni bintiye.
PICHA NA IKULU.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwapisha Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa, ambaye hakuapishwa pamoja na wakuu wa mikoa wenzake Machi 15, 2016.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, uapisho huo umefanyika leo tarehe 28 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Luteni Mstaafu Chiku Gallawa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza kwa Mkoa mpya wa Songwe, ulioanzishwa kwa kuugawa mkoa wa Mbeya, Kusini mwa Tanzania.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu