Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi siku ya jana katika ibada amemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda biblia ya Neno la Mungu kwa makusudi ya kusoma Neno hilo kila siku ili liweze kuwa msaada wake katika shughuli za kila siku za Kiserikali!hivyo kwasasa majukumu na upinzani kwake utakuwa mkubwa zaidi na mwanzo, hivyo anamhitaji Mungu sana Alisema Apostle Ndegi.

Apostle Ndegi aliongeza kwa kusema Mh. Makonda anahitaji maombi ya kila Mtu kwa Mungu ili afanikishe majukumu yake sawasawa.

Mh. Makonda akiongea alisema kila mtanzania kwa nafasi yake lazima ahakikishe anatimiza majukumu yake vizuri tena kwa kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo kwa nafasi ya mtu mmoja na kuacha kutegemea na kusubiri serikali.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Makonda aliongozana na Mke na Mrisho Mpoto katika Ibada hiyo.

Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi

Mrisho Mpoto aliongozana na Mh.Paul Makonda 
Apostle Ndegi akieleza jambo kuhusu Mhe Makonda.
Mrisho Mpoto aliongozana na Mh.Paul Makonda

Apostle Ndegi akimpa maelekezo kuhusu kusoma Neno la Mungu kila siku maana ndio litamsaidia katika shughuli za kila siku

RC Paul Makonda akiwa na mke wake wakikabidhiwa Biblia ya Neno la Mungu 
RC Paul Makonda alipata kuongoza nyimbo ya sifa katika ibada hiyo 
RC Paul Makonda alipata kuongoza nyimbo ya sifa katika ibada hiyo. 


Apostle Ndegi na wachungaji wengine katika Kanisa hilo wakifanya maombi kwa Mh. Paul Makonda
Picha ya pamoja Apostle wa kwanza kushoto, Mhe Makonda, Mke wa Apostle Ndegi ni mke wa Mh. Makonda
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: