UTANGULIZI:

Kufuatiahali ya Amani Zanzibar kuwa mashakani kutokana na mgawanyiko miongoni mwa jamii unaosababishwa na tofauti mbalimbali zikiwemo za kisiasa. Baraza la Viongozi wa Dini mbalimbali kwa Ujenzi wa Amani Tanzania (IRCPT) wamewakutanisha viongozi wa Dini wamadhehebu mbalimbali ya Ukristo na Uislam na Jumuiya ya Hindu kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuzungumzia hali hali si Zanzibar na nini kifanyike kudumisha amani, ambao baada ya majadiliano ya kina wameazimia yafuatayo:

MAAZIMIO:

Kwa kutambua kuwa Zanzibar ni moja na watu wake ni wa moja na amani ni tunu adhimu kwa watanzania wote,

1. Viongozi wa Dini tunawapongeza Watanzania wenzetu wa Zanzibar kwa kuwa wavumilivu nakuilinda Amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi hadi sasa.

2. Viongozi wa Dini, wajitenge na siasa za vyama, kwani wao wanapaswa kua nguzo za jamii zenye Imani na asili tofauti, wasuluhishi na watetezi wa Amani nchini.

3. Vyomba vya usalama, wa wabaini na kuwachukulia hatua vikundi vya uvunjifu wa Amani ili wananchi waishi kwa Amani. (Watumie nguvu inayostahili naisiogopesha umma).

4. Vyama vya siasa vinavyotoa kauli na taarifa zisizo sahihi na kuleta uchochezi. Viache muenendo huo ili kudumisha Amani. Kwani kila mmoja anawajibu wakuitetea Tunu hii ya Taifa.

5. Tume ya Uchaguzi, wawe waadilifu, kusimamia haki, sheria, kanuni na uwazi ilikudumisha Amani katikakipindihiki cha uchaguzi

6. Vyombo vya habari visaidie kuhakikisha tunapita kwenye uchaguzi kwa usalama na amani kwa kutoa taarifa sahihi, kuzingatia maadili na kufuata taratibu na sheria zilizopo.

7. Mahali ambapo uvunjifu wa Amani na wahusika ni dhahiri vyombo vya usalama wachukuliwe hatua stahiki za kisheria.

8. Wananchi ambao pia ni waumini wetu wailinde Amani kutoka mioyo ni mwao, kwanini wajibu wao wa kiroho na kijamii.

9. Wananchi watakaoshiriki kupiga kura wakitumia haki yao ya kimsingi, wahakikishiwe Amani na wale ambao hawatashiriki wasibugudhiwe na wao pia wahakikishiwe Amani.

“ZANZIBAR MOJA, WATU WAKE NI WAMOJA, TUUNGANE KULINDA AMANI KWA MAENDELEO YETU”

“AMANI KWANZA”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: