Vivuko vya Magogoni/Kigamboni vinasimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). 

MV. Magogoni ina uwezo wa kubeba tani 500, ambayo ni sawa na kubeba abiria 2000 na magari madogo 60 kwa wakati mmoja. 

Kivuko hiki kiko katika hali nzuri, kinafanya kazi saa 20 kwa siku, na kupumzika kuazia saa 6:00 usiku mpaka saa 10:00 alfajiri kila siku ili kufanyiwa matengenezo ya kinga (service)
MV. Kigamboni inauwezo wa kubeba tani 160, ambayo ni sawa na kubeba abiria 800 na magari madogo 21 Kwa wakati mmoja. 

Kivuko hiki kinafanya kazi kwa saa 22 kwa siku, na kupumzika kuazia saa 4:00 usiku mpaka saa 6:00 usiku kila siku ili kufanyiwa matengenezo ya kinga (service).

Vivuko hivi husimama muda ambao watumiaji wa vivuko wamepungua na havisimami vyote kwa wakati mmoja ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa kipindi ambacho kivuko kimoja kimesimama. 
Aidha vivuko vya Magogoni/Kigamboni vinakabiliwa na changamoto ya shuguli za kibinadamu zinazofanywa katika eneo la Magogoni Kigamboni, ambazo huchangia uchafuzi wa mazingira ya bahari. 

Uchafuzi huo husababisha takataka kuingia kwenye mifumo ya kuendeshea vivuko (pump jets) na kusababisha mifumo hiyo kushindwa kufanya kazi vizuri. Hali hii imekuwa ikilazimisha vivuko hivyo kusimama muda ambao si wa matengenezo, ili kuondoa taka hizo, kwa lengo la kuepuka uharibifu ambao ungeweza kusababishwa na taka hizo, kama kuharibu mifumo ya kuendeshea vivuko. 

 TEMESA inatoa rai kwa watu wote wanaotumia mazingira ya Magogoni/Kigamboni kuyatunza mazingira hayo, ili kuepusha adha ya usafiri wa vivuko.

Mwisho TEMESA inawashauri watumiaji wa kivuko cha Magogoni/Kigamboni kufuata taratibu zote za kivuko kama inavyoelekezwa ili kutoathiri utoaji wa huduma hiyo. 
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI TEMESA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: