Wednesday, March 23, 2016

WAOMBA SERIKALI KUANGALIA KWA UNDANI MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA KWANI INAKASORO NYINGI

Kutoka Kulia Phidesia Mwakitalima, katibu wa Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya Arusha Rehema Mohamed, Augustino Masawe wawakilishi kamati ya utekelezaji wazazi wilaya ya Arusha wakiwa na Afisa ustawi wa jamii jiji la Arusha Mussa Mkamate katika mazungumzo juu ya Mahabusu ya watoto Arusha.
Picha ikionyesha uchakavu wa vyoo vya mahabusu ya watoto Arusha pamoja na pakti za viroba ambavyo wanakunywa kisiri siri na kuletewa kinyemela na vijana wa mtaani kutokana na kukosa ulinzi kwa mahabusu hayo pia kukosekana kwa uzio katika magereza hiyo ya watoto, na imeonekana pia kuna matundu ya mapaa ya mabati ambayo hayapo pichani Matundu ambayo yamechakaa yanatumika na watoto hao kama njia ya kutorokea nje ambapo mara kadhaa hukamatwa wakiwa wanatoroka na kurudishwa ndani

Na Woinde Shizza, Arusha.

Kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi wilaya ya Arusha inatarajia kutembelea mahabusu ya watoto Arusha katika kuazimisha sherehe ya wiki ya wazazi Tanzania inayofanyika kila april 2 kila mwaka.

Katika maazimisho hayo pia kamati hiyo imejipanga kukarabati baadhi ya miundo mbinu ya kituo cha mahabusu ya watoto iliyopo jijini hapa.

Akizungumzia maadhimisho hayo katibu wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha Rehema Mohamed alisema wao kama wazazi wamegundua kuna changamoto nyingi katika mahabusu ya watoto mkoani Arusha ambazo wazazi kama walezi wameona ni vyema kutembelea mahabusu ya watoto kuwaona na kuwapelekea chochote kinachopatikana .

Alisema kuwa wanajaribu pia kutatua changamoto nyingi wanazokabiliana nazo ili kuweza kuwasaidia watoto hao nao waishi kama watoto wengine walioko majumbani.

“Kwa kweli natoa wito kwa wazazi wote watakaoguswa Arusha kujumuika nasi tar 2 mwezi wa nne kuanzia saa 3kamili asubuhi kwani watoto wengine wazazi wao wamewatelekeza kabisa na wengine hawana wazazi kabisa” alisema Rehema.

Kwa upande wake mjumbe wa Kamati hiyo Phidesia Mwakitalima alisema kuwa Watoto hawa wengine wazazi wao hawaji kuwaona wengine hawana wazazi wanakabiliana na changamoto nyingi sana ikiwemo pia kesi zao kwenda taratibu.

Mwakitalima alisema kwa sababu watoto waliopo katika mahabusu hiyo ni watoto wenye haki ya kupata elimu hivyo pia aliomba serekali ijaribu kuwafikiria watoto hawa ambao wapo mahabusu.

Ameongeza kuwa endapo watoto hao watapatiwa elimu wakiwemo mahabusu  itawasaida kwani hata wakiondoka hapo hawataondoka bure na pia atatoka na elimu ambayo itamsaidia hata akienda nkuondoa ujinga mtaani na pia itamsaidia ata kutoweza kujiingiza katika makundi mabaya ya mtaani kwani atakuwa na elimu kidogo ambayo itamsaida katika maisha yake.

Aidha aliomba serekali pia iangalie mahabusu hiyo kwani watoto wengine kesi zao zinasikilizwa mda mrefu bila suluhu na makosa mengine kisheria likifikishwa mahakamani kesi inapaswa kuisha siku hiyo hiyo  “Mfano hapa kuna kesi ya mauaji mtoto alimsaidia dada yake asichomwe kisu na shemeji yake akachukua kisu akamuwahi shemeji yake na amekubali kosa lakini mwaka wa pili mahakamani wanasema ushahidi haujakamilika hivyo jamani naomba serikali iangalie sana hawa watoto kwani mbali na yote wanateseka wasaidie angalau kesi zao zisikilizwe kwa wakati na watendewe haki jamani kiukweli inauma naomba  serikali iwaangalie awa watoto jamani “alisema Phidesia

Aidha aliomba serikali kuangalia kwa makini sana mahabusu hii ya watoto kwani mbali na hivi pia mahabusu hii watoto wakiumwa wanapelekwa hospital na pikipiki hakuna gari ya mahabusu saa nyingine dawa zinakosekana na maafisa kujikuta wakijipapasa mifukoni mwao kunusuru watoto umauti usiwakute.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu