Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency LTD,Hashim Lundenga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO),kuhusiana na msimu mpya wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016. Lundenga amesema kuwa msimu huo mpya unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumamosi Machi 19, 2016 katika hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar.Katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake Mgeni rasmi amepangwa kuwa ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.Kati ni Mshindi wa Miss Tanzania 2014-2015 Liliani Kamazima pamoja na Mkuu wa Itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye.
Lundega akifafanua jambo kwa umakini mbele ya Wanahabari (hawapo pichani).

Lundenga amesema kuwa katika uzinduzi wa msimu huo mpya,utawakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya Urembo wakiwemo Wabunifu wa Mavazi,Mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini.kama vile haitoshi Lundenga alibainisha kuwa pia Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ambao miongoni mwao wanatarajia kuwa Wadhamini wa shindano hilo kwa mwaka huu.

Katika kunogesha uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake,Lundemga amesema kuwa burudani kadhaa zitakuwepo akiwemo msanii wa kizazi kipya Linah Sanga pamoja na msanii wa ngoma za asili Wanne Star.

Lundenga alisema kuwa mara baada ya uzinduzi huo kufanyika jijini Dar,utahamia mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya uzinduzi," Uzinduzi huo ukikamilika itafuata ratiba ya semina ya mawakala na kuanza kwa mashindano ya urembo katika ngazi za vituo,Wilaya,Mikoa na Kanda",alisema Lundenga.

Amesema kuwa mpaka sasa Wadhamini kadhaa wamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kudhamini shindano hilo katika ngazi ya Taifa.Lundenga ameyataja makampuni ambayo yamedhamini uzinduzi huo wa shindano la urembo la Miss Tanzania 2016 kuwa ni Ramada Resort Dar,Naf Beach hotel Mtwara,Kitwe General Trader,CXC Africa,MMI Tanzania,Mwandago Investment Ltd,Break Point pamoja na GSM Media.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: