Thursday, March 10, 2016

YANAUMA YAMEUGUSA MOYO WANGU... ILA TUTAFIKA!

 Maneno haya kayaandika Laura Pettie, yameugusa moyo wangu sana!

..... Umerudi saa tano usiku nyumbani.... umechoka... unaamua kupumzika labda pasipo hata kuwachungulia wanao... Asubuhi maisha yanakulazimu kuamka alfajiri kuwahi usafiri wa kibaruani!

Unaondoka tena pasipo kuwaona wanao pengine bila kumsemesha mwenza... unasema leo nitawahi kurudi... unasema leo nitawaletea matunda nitakaporudi... unakumbuka na mahitaji yao mengine waliyokwambia jumapili ulipokuwa nyumbani.

Unatoka! unaenda zako! lakini hurudi! hurudi ukiwa hai! hurudi kuwaona wanao! hurudi na matunda wala mahitaji!... unarudi ukiwa ndani ya jeneza!! Ajali kama hii iliyotokea Tabata - Matumbi imekuchukua!

..... Una mipango ya maisha... una ndoto za kutimiza... unaamka alfajiri hii kukimbizia ndoto zako na ghafla ajali kama hii ya leo inachukua mikono yako, inachukua miguu yako, inachukua afya yako... inachukua macho yako... unajikuta mlemavu wa maisha! pengine hata ile akiba ndogo uliyonayo inamalizikia kwenye matibabu!! Hujafa Hujaumbika!

.... Ni mke!.... ni mtoto... ni ndugu... ni rafiki unasubiri msaada mkubwa utakaobadili maisha yako hivi karibuni.... pengine una mipango mikubwa saaaana na mwenzio... ajali kama hii ya leo inavuruga kila kitu pengine inabadili kabisa muelekeo wa maisha yako unarudi chini zaidi ghafla tu!

Rafiki! kila siku unayoishi ni siku mpya... kila muda unaopita ni muda wa nyongeza.... kumbatia kila lililo jema kadiri uwezavyo huwezi jua ya kesho!

Wapumzike kwa amani waliotangulia alfajiri ya leo!... na Mungu awape nafuu majeruhi wote!

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu