Thursday, March 31, 2016

YANGA YATINGA NDANI YA NUSU FAINALI YA FA CUP KWA KUIFUNGA NDANDA FC 2 - 1

Mchezaji wa Yanga, Paul Nonga akiluka kwanja la Mchezaji wa Ndanda FC, Paul Ngalame wakati wa mchezo wao wa Kombe la Shilikisho (FA) uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya FA baada ya kuifunga Ndanda FC kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa Alhamisi March 31 kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam.

Paul Nonga alifunga goli la kwanza dakika ya 27 kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Juma Abdul baada ya Kigi Makasi kumfanyia madhambi Donald Ngoma nje kidogo ya box la penati.

Kigi Makasi mchezaji wa zamani wa Yanga aliisawazishia Ndanda goli hilo kwa shuti kali mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Kelvin Yondani aliifungia Yanga bao lililoipeleka Yanga moja kwa moja kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup. Kelvin alifunga bao hilo kwa penati baada ya Simon Msuva kuangushwa na Paul Ngalema kwenye eneo la penati box na mwamuzi kuamua ipigwe penati ambayo ilifungwa na Yondani.
Mchezaji wa Yanga, Saimon Msuva akiluka kwanja la Mchezaji wa Ndanda FC, Paul Ngalame wakati wa mchezo wao wa Kombe la Shilikisho (FA) uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezaji wa Yanga, Donalid Ngomaakijalibu kuwatokawachezaji wa Ndanda FC, wakati wa mchezo wao wa Kombe la Shilikisho (FA) uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
 Wachezaji wa Timua ya Ndanda FC wakishangilia baada ya baada ya kupata bao dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho FA kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la Ushindi dhidi ya Ndanda FC katiki mchezo wa Kombe la Shirikisho FA kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu