Tuesday, April 5, 2016

DANIEL KIJO NDANI YA BOYS BOYS SEASON 5

 Boys boys ni kipindi kinachorushwa na Tv1 Tanzania kinachokutanisha wanaume na kuzungumza mambo mbali mbali kama mahusiano, elimu, afya, uchumi biashara na mengine mengi. Mbali na hayo unapata fursa ya kuona magari makali , sehemu nzuri za wanaume kupata kinywaji na kupumzika bila kusahau gadgets kali kabisa.

Mtangazajibwa season ya tano atakuwa ni Daniel kijo ambaye ameweza kutumia ujuzi na elimu yake kuboresha na kupanua ufanisi wake katika taaluma ya utangazajaji. Ametumikia jamii katika sekta mbali mbali, lakini kipaumbele chake nikukufikia wewe mtazamaji. Kaa tayari Kwa muonekano mpya wa msimu mpya wa show ya "boys boys" ikiletwa kwenu na Daniel Kijo.

Ijuma hii kipindi cha kwanza msimu wa tano kitaruka saa 2.30 usiku na atakuwepo Godwin Gondwe, Bikira wa Kisukuma na Harmonize wakijadili namna ya kupata mwanamke mwenye kipato zaidi yako.

Usikose!!

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu