Monday, April 18, 2016

DARAJA LA KIGAMBONI KUFUNGWA KESHO JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016 KUPISHA UZINDUZI

MABADILIKO YA MUDA WA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI SIKU YA JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 kuanzia saa mbili asubuhi.

Kufuatia ufunguzi huo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya kutumia daraja hilo itafungwa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nane mchana ili kuwezesha kufanyika kwa hafla ya ufunguzi.

Aidha huduma katika daraja la kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa nane mchana mara baada ya Mheshimiwa Rais kufungua daraja hilo rasmi.

Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa Kilometa 2.5. Ujenzi wake umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
18 Aprili, 2016

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu