Saturday, April 16, 2016

MAANDIKO YASEMAVYO JUU YA NGUVU YA FIMBO NA NIDHAMU KWA MTOTO

1) Mzazi asimnyime mtoto mapigo kwani ni msaada wake wa sasa na baadaye.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

2) Mzazi asiye mchapa mwanaye anapokosea hampendi na humtia katika maisha mabaya ya badaye.

Mithali 13:24
Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

3) Maumivu ya fimbo ndio yanayosafisha uovu wa mtoto kuanzia ndani kuja nje.
• Mtoto asiyechapwa, atakuwa amejaa uchafu wa maovu.
• Fagio la kusafisha maovu ya mtoto ni fimbo.
Mithali 20:30
Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikilia ndani ya mtima.

4) Mtoto anayepewa nidhamu na mzazi huokolewa na kuzimu.
Usipomchapa mwanao pale anapokuwa anakosea, unamuandalia njia ya kwenda kuzimu.
Mithali 23:14
Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

5) Kifaa kinachoondoa upumbavu kwa mtoto ni Fimbo.
• Mjeledi unamfanya farasi aende anakotakiwa.
• Lijamu inamfanya punda aende anakopaswa.
• Fimbo Inamfanya mtoto atembee katika njia impasayo.
Mithali 26:3
Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.

6) Fimbo inaleta hekima kwa mtoto.
• Mtoto anayepata fimbo kutoka kwa mzazi wake atakuwa na hekima na busara.
• Mtoto asiyepata fimbo:
Atajiabisha yeye mwenyewe
Ataaibisha wazazi wake
Ataliaibisha kanisa la Mungu
Ataliaibisha taifa lake pia.
Mithali 29:15
Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu